Duration 5:00

KAMPUNI YA BARRICK YAILIPA SERIKALI DOLA MILIONI 100, WAZIRI WA FEDHA AHUTUBIA HAFLA HIYO

581 watched
0
11
Published 26 May 2020

KAMPUNI ya Barrick imeilipa Tanzania dola milioni 100, sawa na takriban sh. bilioni 250, ikiwa ni sehemu ya malipo ya dola milioni 300 ambazo Kampuni hiyo ya Madini ilikubali kulipa kama fidia ya kodi. Mfano wa Hundi ya kiasi hicho cha fedha imekabidhiwa na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Barrick, Bw. Hilaire Diarra kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, kwa niaba ya Serikali, Jijini Dodoma leo Mei 26, 2020. Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mwenyekiti wa Timu ya Serikali ya Majadiliano na Barrick ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Kamati yake, Dkt. Mpango alisema tukio hilo ni mwanzo wa makubaliano ya mkataba wa msingi kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni hiyo yaliyofikiwa Disemba 19, 2019 na kusainiwa rasmi Januari 24, 2020.

Category

Show more

Comments - 2